Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

NCHI NA WATU

Kutembelea Liechtenstein

Kutembelea Liechtenstein

LIECHTENSTEIN ni moja kati ya nchi ndogo zaidi duniani. Nchi hiyo iko kwenye milima ya Alps katikati ya Uswisi na Austria. Waselti, Waraetia, Waroma, na Waalemani wamewahi kuishi hapo. Leo, karibu robo tatu ya wakazi wa Liechtenstein ni wazawa wa kabila la Waalemani, ambao wameishi hapo kwa miaka 1,500 hivi.

Lugha kuu inayozungumzwa Liechtenstein ni Kijerumani, hata hivyo lahaja hutofautiana kati ya kijiji kimoja na kingine. Baadhi ya vyakula vya asili ni Tüarka-Rebel, kinachotengezwa kwa kutumia mahindi, na Käsknöpfle, yaani, tambi zenye jibini.

Käsknöpfle

Mavazi ya kitamaduni yenye rangi mbalimbali

Watalii wanapotembelea eneo hilo wao huona milima iliyofunikwa na theluji, mabonde ya kijani, mashamba ya mizabibu, na mimea mbalimbali. Kwa mfano, kuna karibu aina 50 za okidi za msituni katika nchi hiyo ndogo. Pia, kuna majumba ya makumbusho, kumbi za sinema, na viwanda vya kutengeneza divai. Hivyo, watalii hutembelea nchi hiyo kila wakati, iwe kuna majira ya kiangazi au ya baridi kali.

Mashahidi wa Yehova wamekuwapo nchini humo tangu miaka ya 1920. Kwa sasa, kuna Mashahidi 90 hivi nchini humo, wanaowafundisha Biblia wageni na wenyeji.