Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

Njia ya Maziwa

Njia ya Maziwa

Je, Ni Kazi ya Ubuni?

Njia ya Maziwa

▪ Ikiwa umewahi kutazama kondoo, mbuzi au ng’ombe wanapozaa, huenda ulishangaa kuona jinsi watoto wao waliotoka tu kuzaliwa wanavyosimama baada ya muda mfupi na kuanza kunyonya. Mamalia wote huwanyonyesha watoto wao. Lakini kuna jambo lingine linalostaajabisha kuhusu watoto wa wanyama wanaocheua, kama vile wana-kondoo, wana-mbuzi, na ndama.

Fikiria hili: Ng’ombe wana tumbo lenye sehemu nne la kumeng’enya nyasi na mimea mingine. Lakini ndama hunywa maziwa ambayo hayahitaji kupitia hatua zote za umeng’enyaji. Kwa hiyo, ndama anaponyonya, njia fulani ya pekee hufanya maziwa yaende moja kwa moja hadi sehemu ya mwisho ya tumbo.

Ikiwa maziwa yangeingia kwenye sehemu ya kwanza ya tumbo (rumen), ndama angeathiriwa kwa sababu sehemu hiyo humeng’enya chakula kigumu kwa kutumia bakteria zinazokichachisha. Maziwa yaliyochacha yanatokeza gesi ambayo ndama hawawezi kuitoa. Hata hivyo, watoto wa wanyama wanaocheua wanapokunywa maziwa, iwe ni kwa kunyonya au kutoka kwenye ndoo, msuli fulani hufunga njia ya kuingia kwenye sehemu ya kwanza ya tumbo.

Kwa kustaajabisha, mambo yanakuwa tofauti ndama anapokunywa maji. Ndama anahitaji maji mengi katika sehemu ya kwanza ya tumbo ili bakteria na vijidudu viongezeke kwa ajili ya wakati atakapoanza kula mimea. Ingawa maziwa huenda moja kwa moja kwenye sehemu ya mwisho ya tumbo, maji huingia kwenye sehemu ya kwanza ya tumbo. Ndama hupitisha maziwa peke yake kupitia hiyo njia ya pekee!

Una maoni gani? Je, njia ya maziwa ilijitokeza yenyewe? Au je, ni kazi ya Muumba mwenye akili?

[Mchoro/Picha katika ukurasa wa 13]

 

Maziwa hayaingii kwenye sehemu tatu za kwanza katika tumbo la ndama

[Mchoro]

Njia ya maziwa

1 Rumen

2 Reticulum

3 Omasum

4 Abomasum (sehemu ya mwisho ya tumbo)