Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

Mfumo wa Kujisukuma wa Kiwavi wa Baharini

Mfumo wa Kujisukuma wa Kiwavi wa Baharini

Je, Ni Kazi Ya Ubuni?

Mfumo wa Kujisukuma wa Kiwavi wa Baharini

● Asilimia 95 ya mwili wa kiwavi wa baharini ni maji na wanaweza kuwa na kipenyo cha sentimita 3 hadi mita 2. Jamii nyingi za viwavi hao hutumia misuli kujisukuma kwa kukaza na kulegeza mwili wao ulio na umbo kama la kengele, kama vile mtu anavyokunja na kukunjua mwavuli.

Fikiria hili: Wanasayansi ambao huchunguza jinsi gesi na umajimaji husonga wamegundua kwamba aina fulani za viwavi wa baharini, ingawa hawawezi kuogolea kwa kasi, wana mbinu yenye kustaajabisha ya kujisukuma. Kila wakati mwili wao unapojikaza, wanyama hao hufanya maji yatokeze umbo la mviringo lenye shimo katikati kama la tairi ya gari, na hivyo wanajisukuma. Msukumo unaotokezwa huwafanya viwavi hao kusonga mbele, kama ndege ya abiria inayosonga hatua kwa hatua. Gazeti New Scientist linasema, “huenda jambo hilo likaonekana kuwa rahisi, lakini tendo la kufanya maji yatokeze umbo la mviringo lenye shimo katikati ni gumu sana hivi kwamba haliwezi kufafanuliwa kwa kutumia hisabati.”

Watafiti wanachunguza mfumo wa kujisukuma wa kiwavi wa baharini ili watengeneze vyombo vinavyoweza kusonga chini ya maji kwa njia bora zaidi. Mtafiti mmoja tayari amebuni nyambizi yenye urefu wa mita 1.2 ambayo husonga kwa njia kama ile inayotumiwa na kiwavi wa baharini. Nyambizi hiyo inatumia nishati kidogo zaidi kwa asilimia 30 ya nishati inayotumiwa na nyambizi za kawaida. Mbinu hiyo pia inaweza kutumiwa katika moyo wa mwanadamu. Kwa sababu damu katika sehemu fulani ya moyo husonga kwa njia kama ile inayotumiwa na kiwavi huyo, ugonjwa wa moyo unaweza kutambuliwa mapema sana.

Una maoni gani? Je, mbinu ya kujisukuma ya kiwavi wa baharini ilijitokeza yenyewe? Au ilibuniwa?

[Picha katika ukurasa wa 13]

Viwavi wa baharini hufanyiza umbo linalowasaidia kujisukuma

[Hisani ya Picha katika ukurasa wa 13]

Photo: © JUNIORS BILDARCHIV/age fotostock; graphic: Courtesy of Sean Colin