Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

WIMBO NA. 82

“Acheni Nuru Yenu Iangaze”

“Acheni Nuru Yenu Iangaze”

(Mathayo 5:16)

  1. 1. Yesu aamuru,

    Twangaze nuru.

    Bila ubaguzi,

    Wote waone.

    Neno lake Mungu,

    Liwape nuru.

    Tufundishapo Neno,

    Twangaze nuru.

  2. 2. Tunapotangaza

    Habari njema.

    Neno lake Mungu,

    Latuongoza.

    Linawapatia,

    Wote nafasi.

    Wachague wenyewe,

    Toka moyoni.

  3. 3. Tufanyapo mema,

    Nuru yang’aa.

    Fundisho la Bwana,

    Tunalipamba.

    Tunampendeza,

    Yehova Mungu.

    Tuangaze daima,

    Nuru ya kweli.