Hamia kwenye habari

Awamu ya 8 ya Picha za Uingereza (Machi Hadi Agosti 2019)

Awamu ya 8 ya Picha za Uingereza (Machi Hadi Agosti 2019)

Katika awamu hii ya picha, utaona jinsi ujenzi ulivyoendelea katika ofisi mpya ya tawi ya Mashahidi wa Yehova nchini Uingereza kati ya Machi na Agosti 2019.

  1. Jengo la Kaskazini la (Utayarishaji wa Video)

  2. Jengo la Kusini la (Udumishaji na Huduma)

  3. Jengo la Ofisi

  4. Makazi A

  5. Makazi B

  6. Makazi C

  7. Makazi D

  8. Makazi E

  9. Makazi F

Machi 5, 2019—Jengo la Ofisi

Mfanyakazi akifunika mabomba ya kupashia joto kwa vifaa maalumu katika chumba cha matangi ya kupashia joto.

Machi 29, 2019—Jengo la Kusini Udumishaji na Huduma

Wanaume wenye ujuzi wakiweka vigae kwenye kuta za bafu zilizo katika vyumba vya kubadilishia mavazi.

Aprili 10, 2019—Jengo la Ofisi

Mfanyakazi akiweka viunzi vya mfumo wa kujilinda dhidi ya radi. Mfumo mzima umebuniwa kulinda jengo lote radi inapopiga. Ili kufanya kazi kwa usalama zaidi, mfanyakazi huyu ana kamba kiunoni iliyofungwa kwenye paa.

Aprili 16, 2019—Jengo la Ofisi

Wanasafisha madirisha ili vibandiko vya usalama viwekwe. Vibandiko hivyo vinafanya vioo hivi vikubwa vionekane, ili kuzuia watu wasigonge vioo hivyo bila kujua

Aprili 23, 2019—Makazi A

Mfanyakazi anatumia mfumo wa video kuhakikisha kwamba mabomba yote ya kuondoa maji-taka yako tayari.

Aprili 23, 2019—Jengo la Ofisi

Mafundi seremala wakiunganisha vipande vya mbao kwenye kuta za eneo ambalo linaweza kutumika kwa ajili ya shughuli mbalimbali kama vile kulia chakula na ukumbi wa mikutano. Matukio ya pekee pia yatafanyiwa katika eneo hili pia.

Mei 14, 2019—Makazi B

Wafanyakazi wa bustani wakipanda maua karibu na ukuta.

Mei 14, 2019—Makazi A

Wafanyakazi wa mapambo ya nje wakiweka uzio wa kioo mbele ya madirisha, na kutengeneza roshani inayoitwa Juliet. Uzio huu huwalinda wakazi bila kuzuia mwanga au hewa.

Mei 21, 2019—Jengo la Ofisi

Mafundi umeme wakiweka taa mbele ya eneo la mapokezi.

Juni 11, 2019—Jengo la Kaskazini la Utayarishaji wa Video

Mmoja wa mafundi bomba akikata bomba la kupitishia hewa kwa kutumia mkasi maalumu.

Juni 17, 2019—Jengo la Ofisi

Wafanyakazi wa bustani na wa maeneo ya ujenzi wakipanda miti na kutayarisha vijia vya wanaotembea kwa miguu. Upande wa kushoto ni sehemu inayoweza kubadilishwa na kutumiwa kwa ajili ya shughuli mbalimbali kama vile chumba cha kulia chakula, ukumbi, na matukio ya pekee. Jengo la Makazi A linaonekana kwa nyuma.

Juni 24, 2019—Makazi A

Mkandarasi akitengeneza sehemu ya mfumo wa kuzima moto.

Julai 9, 2019—Jengo la Ofisi

Wafanyakazi wa bustani wanaandaa ardhi kwa ajili ya kupanda mbegu za nyasi. Kwa nyuma madirisha ya ofisi yanasafishwa kwa kutumia mfumo rahisi wa kusafisha madirisha.

Julai 9, 2019—Jengo la Kaskazini la Utayarishaji wa Video

Wafanyakazi wakiweka mchanganyiko fulani wa kemikali katika sakafu unaosaidia kusawazisha sakafu. Wanatumia reki ya pekee ili kuhakikisha mchanganyiko huo umeenea kote kwa usawa, kisha wanatumia brashi zenye meno ili kuondoa viputo vya hewa.

Julai 24, 2019—Jengo la Ofisi

Wafanyakazi wakitandika sakafu maalumu katika chumba cha kulia chakula kinachoweza kubadilishwa na kutumiwa kama ukumbi, au kwa ajili ya matukio ya pekee. Skrini za televisheni zimewekwa kwenye ukuta ambao jukwaa litakuwepo.

Julai 26, 2019—Jengo la Kaskazini la Utayarishaji wa Video

Pembeni ya studio ya video, fundi seremala anatengeneza chumba cha saluni kitakachotumiwa na wale watakaoshiriki kuigiza katika video.

Agosti 1, 2019—Jengo la Kaskazini la Utayarishaji wa Video

Mafundi seremala wakiunganisha vipande vya mbao vitakavyotumiwa kutenganisha ofisi. Vipande hivyo vitaruhusu idara mbalimbali kubadilisha mwonekano wa ofisi kwa urahisi ikitegemea uhitaji.

Agosti 1, 2019—Jengo la Kaskazini la Utayarishaji wa Video

Mkandarasi akiunganisha vyuma vitakavyotumiwa kutengeneza studio ya video. Vyuma hivyo hutumika kuning’iniza vifaa kama vile taa na kamera wakati wa kutayarisha video.

Agosti 15, 2019—Eneo la ujenzi wa Ofisi ya Tawi

Picha iliyopigwa kutoka upande wa kaskazini. Upande wa kushoto, majengo ya Makazi B, C, D, E, na F yamekamilika. Katikati, jengo la Makazi A linakaribia kumalizika na jengo la Ofisi limekamilika tayari. Upande wa kulia, Jengo la Kusini la Udumishaji na Huduma na Jengo la Kaskazini la Utayarishaji wa Video, yanakaribia kumalizika. Wakati huohuo, kazi ya kutengeneza mwonekano wa nje na bustani inaendelea katika eneo lote la ujenzi.

Agosti 26, 2019—Jengo la Ofisi

Wafanyakazi wakiweka vigae vya mawe kwenye eneo la kutembelea nyuma ya eneo la mapokezi. Mahema yanayoonekana kwa nyuma yanatumiwa kama kivuli wafanyakazi wanaposafisha vigae vipya vinavyowekwa.