Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

 NCHI NA WATU

Kutembelea Panama

Kutembelea Panama

PANAMA inajulikana sana kwa sababu ya mfereji wake unaounganisha bahari ya Atlantiki na Pasifiki. Lakini kwa sababu inaunganisha mabara ya Amerika Kaskazini na Amerika Kusini, Panama pia inaunganisha watu. Nchi hiyo ina watu wa jamii na utamaduni mbalimbali. Asilimia kubwa ya watu ni mchanganyiko wa wenyeji na wazungu.

JE, WAJUA? Chura wa Panama mwenye rangi ya dhahabu (Atelopus zeteki) “hupunga” miguu yake ya mbele ili kuvutia wenzi watarajiwa na kuwaonya vyura wengine

Katika mwaka wa 1501, wavumbuzi Wahispania walipowasili Panama, walikuta jamii nyingi sana za wenyeji, na baadhi ya hizo zipo mpaka leo. Jamii moja inaitwa Guna (awali iliitwa Kuna). Waguna wengi wanaishi katika eneo la wenyeji la visiwa vya San Blas na kandokando ya Pwani ya Karibea karibu na mpaka wa Panama na Kolombia. Huko, wao huwinda,  huvua samaki wakiwa katika mitumbwi, na wanakuza chakula chao wenyewe.

Katika jamii ya Waguna, mwanamume anapooa, yeye huenda kuishi na familia ya mke wake na kuwafanyia kazi. Mke wake anapojifungua mtoto wa kike, ndipo tu ataondoka na familia yake kutoka kwa wakwe zake akatafute makao yake mwenyewe.

Kuna makutaniko karibu 300 ya Mashahidi wa Yehova nchini Panama. Mbali na Kihispania, mikutano inafanywa pia katika Kichina, Kiingereza, Kigujarati, Kiguna, Kikrioli cha Haiti, Kingabere, na Lugha ya Ishara ya Panama.