Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

MAISHA YA MKRISTO

Ni Nani Marafiki Wako Mtandaoni?

Ni Nani Marafiki Wako Mtandaoni?

Rafiki anafafanuliwa kuwa “mtu anayeshikamana na mwingine kwa sababu ya upendo au heshima.” Kwa mfano, Yonathani na Daudi walianzisha urafiki usiovunjika baada ya Daudi kumuua Goliathi. (1Sa 18:1) Kila mmoja wao alionyesha sifa zilizomvutia mwenzake. Hivyo, urafiki wenye nguvu unategemea ujuzi sahihi. Kwa kawaida kumfahamu mtu mwingine huchukua muda na jitihada. Hata hivyo, kwenye mitandao ya kijamii, watu wanaweza kuwa “marafiki” kwa kubofya kitufe tu. Kwa sababu watu mtandaoni wanaweza kupanga kihususa kabisa watasema nini na kudhibiti wengine wanawaonaje, ni rahisi kuficha jinsi walivyo hasa. Hivyo, ni vizuri kuwa mteuzi unachagua watu wa aina gani kuwa marafiki wako. Usiogope kupuuza au kukataa maombi ya watu fulani ya kuwa marafiki ikiwa huwafahamu vizuri eti tu kwa sababu unaogopa utaumiza hisia zao. Kwa sababu ya hatari zinazoweza kutokea, baadhi ya watu wamechagua kutotumia mitandao ya kijamii kabisa. Hata hivyo, ukichagua kutumia mtandao wa kijamii, unapaswa kuzingatia nini?

TAZAMENI VIDEO YENYE KICHWA TUMIA MITANDAO YA KIJAMII KWA HEKIMA, KISHA MJIBU MASWALI YAFUATAYO:

  • Unapaswa kufikiria nini kabla ya kuandika maelezo au kupachika picha?

  • Kwa nini unapaswa kuchagua marafiki wako wa mtandaoni kwa uangalifu?

  • Kwa nini unapaswa kuweka mipaka ya muda unaotumia kwenye mtandao wa kijamii?​—Efe 5:15, 16