Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

Je, Wajua?

Je, Wajua?

Je, Wajua?

Kwa nini Mungu alichagua kware ili kuwalisha Waisraeli nyikani?

Baada ya Waisraeli kutoka Misri, Mungu aliwaandalia kware wengi sana kama chakula, naye alifanya hivyo mara mbili.—Kutoka 16:13; Hesabu 11:31.

Kware ni ndege wadogo, wenye urefu wa sentimita 18 hivi na uzito upatao gramu 100. Wanazaana katika maeneo mengi ya Asia magharibi na Ulaya. Kwa kuwa kware ni ndege wa kuhama-hama, wao huhamia Afrika Kaskazini na Arabia wakati wa baridi kali. Wakati wa kuhama, kware wengi sana huvuka fuo za mashariki za Bahari ya Mediterania na Rasi ya Sinai.

Kulingana na kamusi ya The New Westminster Dictionary of the Bible, kware “wanaruka vizuri na kwa haraka, huku wakisaidiwa na upepo; lakini mkondo wa upepo unapobadilika, au wanapochoka kwa sababu ya safari ndefu, wote huanguka chini na kubaki hapo wakiwa wameshtuka.” Kabla ya kuendelea na safari yao, lazima wapumzike hapo chini kwa siku moja au mbili, hivyo, inakuwa rahisi kwa wawindaji kuwanasa. Mapema katika karne ya 20, Misri ilikuwa inauza kware milioni tatu hivi kila mwaka katika nchi za nje kama chakula.

Pindi mbili ambazo Waisraeli walikula kware, ilikuwa ni majira ya kuchipua. Ingawa kware walivuka kwa ukawaida eneo la Sinai wakati huo, Yehova ndiye aliyefanya ‘upepo uvume’ ili kuwaleta ndege hao kwenye kambi ya Waisraeli.—Hesabu 11:31.

“Sherehe ya wakfu” inayotajwa kwenye Yohana 10:22 ni gani?

Zile sherehe tatu ambazo Mungu aliwaamuru Wayahudi waadhimishe kila mwaka—Sherehe ya Keki Zisizo na Chachu, Sherehe ya Pentekoste, na Sherehe ya Kukusanya—zilifanywa Machi/Aprili, Mei/Juni (Mwezi wa 5 au wa 6), na Septemba/Oktoba (Mwezi wa 9 au wa 10). Hata hivyo, sherehe inayotajwa kwenye Yohana 10:22, ilifanywa “wakati wa majira ya baridi kali” ili kuadhimisha kuwekwa wakfu tena kwa hekalu la Yehova mwaka wa 165 K.W.K. Ilifanywa kwa siku nane, kuanzia siku ya 25 ya mwezi wa Kislevu, karibu na siku ambapo mchana unaanza kuwa mrefu. Kwa nini sherehe hiyo ilianzishwa?

Katika mwaka wa 168 K.W.K., Antioko wa Nne (Epifane), aliyekuwa mtawala wa Siria kutoka ukoo wa Seleuko, aliamua kuondoa kabisa ibada na desturi za Wayahudi, hivyo akajenga madhabahu ya kipagani juu ya madhabahu ya Yehova katika hekalu huko Yerusalemu. Alitumia madhabahu hiyo kutoa dhabihu kwa Zeu, mungu wa Wagiriki.

Jambo hilo lilichochea uasi wa Wamakabayo. Kiongozi wa Wayahudi, Yudasi Makabayo aliuteka tena mji wa Yerusalemu kutoka kwa Waseleuko, kisha akaagiza madhabahu iliyokuwa imetiwa unajisi ibomolewe na nyingine mpya ijengwe mahali hapo. Miaka mitatu kamili baada ya ile madhabahu ya kwanza kutiwa unajisi, Yudasi aliliweka hekalu wakfu tena kwa Yehova, likiwa safi. Tangu wakati huo, Wayahudi wanasherehekea “Sherehe ya wakfu” (Kiebrania, chanuk·kahʹ) mnamo Desemba (Mwezi wa 12). Leo sherehe hiyo inaitwa Hanuka.

[Picha katika ukurasa wa 14]

Picha ya Yudasi Makabayo, Lyon, 1553

[Picha katika ukurasa wa 14]

From the book Wood’s Bible Animals. 1876