Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

Hatuachi

Hatuachi

Pakua:

  1. 1. Nilipoujua ukweli

    Kumhusu Mungu nayo Paradiso.

    Niliupenda na kuthamini.

    Japo ulimwengu wakengeusha.

    (KIBWAGIZO)

    Sitakubali.

    Nitayafanya mema.

    (KORASI)

    Nitaimarisha imani yangu.

    Daima sitayumbishwa.

    Neno Lake ni mwongozo wangu.

    Nasali niwe imara.

    Kujenga imani; sitaacha.

  2. 2. Hivyo lazima tuamue;

    Kuwa imara sio dhaifu.

    Ulimwengu unatudanganya

    Hakuna matata mambo ni shwari.

    (KIBWAGIZO)

    Twajua kweli,

    Mambo ya Ufalme.

    (KORASI)

    Na tuimarishe imani yetu.

    Kamwe hatutayumbishwa.

    Neno Lake ni mwongozo wetu.

    Twasali tuwe imara.

    Kujenga imani hatuachi.

    (KORASI)

    Na tuimarishe imani yetu.

    Kamwe hatutayumbishwa.

    Neno Lake ni mwongozo wetu.

    Twasali tuwe imara.

    Kujenga imani hatuachi.

    Hatuachi.

    Hatuachi.